Takwimu kutoka shirika la chakula na kilimo duniani(FAO) za mwenendo wa masoko ya zao la mahindi katika nchi za mashariki na kusini mwa afrika(2018) kupitia kanzu data yake maarufu ya FAOSTAT, zimeonyesha nchi za Tanzania, Ethiopia, Malawi na Zambia zinaongoza kwa uzalishaji wa mahindi. Kutokana na kubadilika kwa bei ya mahindi kulingana na uhitaji na uzalishaji katika nchi hizo, nchi za Malawi, Zimbabwe, Msumbiji, Ethiopia, Kenya na Burundi zimeonyesha kuwa na wastani wa bei nzuri ya mahindi kutokana na kuwepo kwa ongezeko la uhitaji wa chakula katika nchi hizo kadri siku zinavyokwenda.
Nchi nyingine barani afrika ambayo imeonyesha kuwa na bei nzuri ni Togo, ambayo kutokana na eneo na uhitaji wa chakula kuwa mkubwa bei ya mahindi imeonekana kuwa na wastani wa kupanda hadi kufikia $453(Sawa na wastani wa Tsh 1,010,190) kwa Tani 1 ya mahindi.
Jedwali(Youth Employment in Sub Saharan Countries, World Bank)